Mkuu wa Chuo cha Ualimu Nyamahanga Wiliyani Biharamulo mkoani Kagera anatangaza nafasi za kujiunga na mafunzo ya astashahada ya Elimu ya msingi kwa mwaka wa masomo 2018-2019 (Ualimu daraja A) kwa waliohitimu kidato cha nne kwa ufaulu usiopungua daraja la tatu.
Kozi itakuwa ya miaka miwili ya Ualimu daraja A.Chuo kilisajiliwa mwaka 2006 kikiwa na lengo la kutoa elimu na maadili mema na hadi sasa Chuo kimehitimisha jumla ya walimu elfu moja miatano thelathini na tatu wa daraja A.
Chuo cha Ualimu Nyamahanga kipo umbali wa kilomita tisa kutoka Biharamulo Mjini kwenye barabara ya kuelekea Lusahunga na kipo chini ya Kanisa la Free Pentecostal Church of Tanzania.
Kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia anuani zifuatazo:
Chuo cha Ualimu Nyamahanga
S.L.P 25
Biharamulo-Kagera Tanzania
AU Wasiliana na Mkuu wa Chuo Ndugu BK OBED BYARUGABA Kwa simu namba:0688381381/0753956361
Mtaa wa Bomani
Sanduku la Barua: S.L.P 70
Telephone: 028 2223403
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@biharamulodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya Biharamulo. Haki zote zimehifadhiwa