Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo imepokea shilingimilioni miatano kutoka Hazina kwa
ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya. Taarifa hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa
Wilaya Bi.Wende I. Ng’ahara alipokuwa akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo
robo ya tatu kwenye kikao cha baraza la Madiwani leo.
Amesema fedha hizo ni sehemu ya billion moja, mia tano million zilizotengwa kugharimia ujenzi wa
Hospitali ya Wilaya. Amesema OR-TAMISEMI ilitoa mwongozo wa ujenzi wa Hospitali hiyo ambao
pamoja na maelekezo mengine umeelekeza uundaji wa kamati za ujenzi kwa kutumia “Force Accaunt”
Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya Bi.Wende I. Ng’ahara amesema ujenzi huo utasimamiwa kwa ukaribu na
kufanyika kwa kuzingatia muda, viwango vilivyowekwa katika michoro ili kupata dhamani halisi ya fedha.
Amesema majengo yanayotarajiwa kujengwa ni pamoja na Jengo la utawala, Jengo la wagonjwa wa nje yaani
(OPD), Stoo ya dawa, Maabara,Jengo ya vipimo vya mionzi(x-ray),Jengo la kufulia nguo(Laundry) na
jengo la wazazi. Hospitali hiyo itajengwa Kata ya Nyarubungo Kijiji cha Katoke karibu na eneo za Zahanati ya
Katoke ambalo lilitolewa na Jimbo la Rulenge- Ngara ambalo lilikuwa eneo la Kanisa Katoloki tangu miaka ya
1897 ambapo awali Askofu wa Jimbo la Rulenge Ngara Mhashamu Severine NIWEMUGIZI (SEVERINUS
NIWEMUGIZI EPISCOPUS RULENGENSIS NGARENSIS) alisema anatoa eneo hilo ili litumike kadri ya
mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo.Eneo hilo lina ukubwa wa ekari thelathini na moja (31)
Mtaa wa Bomani
Sanduku la Barua: S.L.P 70
Telephone: 028 2223403
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@biharamulodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya Biharamulo. Haki zote zimehifadhiwa