Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo Bi, Wende Israel Ng’ahara, amesema Mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi (PSLE) 2019 utafanyika tarehe 11/9/2019 hadi 12/9/2019 siku ya jumatano na alhamisi kwa mujibu wa ratiba iliyo tolewa na Baraza la Mitihani Tanzania.
Amesema mwaka huu wa 2019 Wilaya inazo shule 88 zitakazo fanya Mitihani sawa sawa na mwaka 2018 kwa sababu hakuna ongezeko la Shule yoyote.
Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya amesema mwaka huu kuna mikondo 211 yenye watahiniwa 4,591 wakiwa ni Wavulana 2,233 na Wasichana 2,358, tofaut na mwaka 2018 ambapo kulikua na mikondo 191 yenye watahiniwa 4,246 Wavulana 1,992 na Wasichana 2254
Aidha amesema mchanganuo wa watahiniwa katika mfumo wa Kiswahili na mfumo wa Kingereza medium ni kama ifuatavyo,
Watahiniwa wa mfumo wa Kiswahili ni katika shule 85 zenye Wavulana 2,190 Wasichana 2,309 jumla 4,499 sawa na mikondo 206. Amesema mwaka huu hakuna mwanafunzi mwenye uono hafifu.
Ameendelea kusema kuwa watahiniwa wa mfumo wa Kingereza (English Medium) ni Shule tatu ambazo ni St.Severine, Upendo English Medium na Victory English Medium zenye Wavulana 43 na Wasichana 49 jumla 92 sawa na mikondo mitano.
Aliendelea kusema kuwa matokeo ya Mtihani mwaka jana hakuna watahiniwa walio futiwa Mtihani katika Wilaya ya Biharamulo -hii ikimanisha hakukuwa na tuhuma za udanganyifu
Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya amethibitisha kuwa matokeo ya mwaka jana 2018 tulifaulisha kwa asilimia 91.6% ambapo Wilaya ilikuwa ya kwanza Kimkoa na ya kumi na moja Kitaifa ikilinganishwa na mwaka 2017 ambapo Wilaya ilifaulisha kwa asilimia 87.66% ikishika nafasi ya pili Kimkoa na nafasi ya kumi na tisa Kitaifa.
Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano BIHARAMULO
Mtaa wa Bomani
Sanduku la Barua: S.L.P 70
Telephone: 028 2223403
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@biharamulodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya Biharamulo. Haki zote zimehifadhiwa