Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kwa mwaka huu 2019 Ndugu Mzee Mkongea Ally amekataa kuzindua miradi miwili Wilayani Biharamulo baada ya kuwa na wasiwasi juu ya utekelezaji wa miradi hiyo.
Kiongozi huyo amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo Bi. Saada Malude kukabidhi mikataba ya miradi hiyo TAKUKURU ili uchunguzi ufanyike na apewe taarifa haraka sana.
Miradi hiyo ni Mradi wa Maji Ng’ambo ambao thamani yake fedha za Kitanzania ilikuwa millioni mia nne, Mia tano na nane elfu na mianne, fedha hizi zimetolewa na Serikali kupitia Wizara ya Maji.
Mradi wa pili ni mradi wa ujenzi wa Barabara ya lami kilometa moja(Km 1) ambao thamani yake fedha za Kitanzania ilikuwa million mia mbili tisini na nane, mia moja themanini na sita elfu,Mkandarasi wa mradi huu ilikuwa Kampuni ya Kajuna kutoka Wilayani Muleba.
Kufuatia maagizo hayo Ofisi ya TAKUKURU inawashikilia Meneja wa TARULA Eng. M. Lugw’echa Masuka na Meneja wa Mamlaka ya Maji Biharamulo Mjni Ndg. Siraji Athumani Basiga kwa mahojiano zaidi.
Hata hivyo kiongozi huyo wa mbio za mwenge wa uhuru amepongeza miradi mitatu iliyotekelezwa vizuri miradi hiyo ni mradi bweni na vyumba vya madasa shule ya msingi Kabindi Kata ya Kabindi,Shamba la migomba Kata ya Nyabusozi na ujenzi wa Wodi ya akinamama,watoto,Chumba cha kuhifadhia maiti,Maabara na nyumba ya mtumishi Kata ya Nemba.
Imetolewana kitengo cha Habari na Mawasiliano Biharamulo.
Mtaa wa Bomani
Sanduku la Barua: S.L.P 70
Telephone: 028 2223403
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@biharamulodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya Biharamulo. Haki zote zimehifadhiwa