Waziri wa Tawala za Mikoa na Serilikali za Mitaa TAMISEMI Seleman Jafo amewataka viongozi wa Wilaya ya Biharamulo
kusimamia ujenzi wa vyumba vya madarasa unaoendelea kwenye shule mbalimbali ili uweze kukamilika kwa wakati kwa ajili ya
watoto wanaotarajia kuanza masomo mwaka huu.
Aidha, kupitia ofisi wamepanga kukamilisha ujenzi wa miundombinu ya Hosptali ya Wilaya inayojengwa kata ya Nyarubungo na
kuhakikisha wanaweka vifaa Tiba na kujenga shule mbili za Sekondari ili kusaidia wanafunzi wanaotembea umbali mrefu
kufuata shule.
Hata hivyo Waziri Jafo ametembelea shule ya msingi Munzani iliyopo kata ya Nyakahura kwa lengo la kukagua vyumba viwili
vya madarasa vilivyojengwa kwa gharama zaidi ya Tsh. million 400 kwa fedha za mradi wa EP4R na kupongeza wananchi ushilikiano wao
Mtaa wa Bomani
Sanduku la Barua: S.L.P 70
Telephone: 028 2223403
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@biharamulodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya Biharamulo. Haki zote zimehifadhiwa