Wananchi Wote,
TANZANIA BARA.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya Biharamulo inatangaza nafasi mbili (2) zakazi za Watendaji wa Vijiji III.
1. Sifa za mwombaji:-
i. Awe amehitimu na kufaulu Elimu ya kidato cha nne
ii. Awe amehitimu mafunzo ya astashahada / cheti katika mojawapo ya fani za
Utawala,Sheria, Elimu ya jamii, Maendeleo ya jamii na Sayansi ya Sanaa.
2. Ngazi ya Mshahara
Mwombaji atakayefanikiwa kuajiriwa kama Mtendaji wa Kijiji atalipwa mshahara wa viwango vya Serikali katika ngazi ya Mshaharawa TGS B kwa Mwezi.
3. Masharti ya Jumla
Mwombaji anatakiwa kuambatisha:-
i. Nakala ya vyeti vya mafunzo.
ii. Maelezo binafsi (Curriculum Vitae)
iii. Picha ndogo za rangi mbili (passport Size)
iv. Cheti cha kuzaliwa.
N.B. Maombi yote yatumwe kupitia posta kwa anuani ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri ya Wilaya S.L.P 70, Biharamulo.
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 29/08/2019 saa 9:30 alasiri siku ya Alhamisi.
Mtaa wa Bomani
Sanduku la Barua: S.L.P 70
Telephone: 028 2223403
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@biharamulodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya Biharamulo. Haki zote zimehifadhiwa