FURSA ZA UWEKEZAJI KATIKA WILAYA YA BIHARAMULO
MAELEZO MAFUPI YA WILAYA
Mipaka
•Wilaya ya Biharamulo Upande wa Kaskazini inapakana na wilaya za Muleba na Karagwe
•Kusini Wilaya za Kakonko na Bukombe
• Magharibi Wilaya ya Ngara na
•Mashariki Wilaya ya Chato
Jiografia
•Wilaya ipo umbali wa Kilometa 171 kutoka Makao Makuu ya Mkoa (Manispaa ya Bukoba)
•Inapatikana kati ya 2˚15’-3 ˚15’Kusini mwa Ikweta na 31 ˚-32 ˚ Mashariki mwa “Standard Meridian
Hali ya Hewa
•Wilaya inajotoridi la wastani wa 27 ˚C
•Wilaya ya Biharamulo hupata mvua kati ya mm 700 hadi 1000 kwa mwaka ikiwa ni wastani wa siku 110 kwa mwaka
•Kiwango hiki cha mvua kinaruhusu kusitawisha aina mbalimbali za mazao
Utawala
•Wilaya imegawanyika katika Tarafa 2 , Kata 17 na vijiji 75 na vitongoji 374
•Wilaya ina jimbo 1 la uchaguzi
•Wilaya ina Waheshimiwa Madiwani 24
Idadi ya Watu
• Wilaya ya Biharamulo inakadiriwa kuwa na watu 461,346 (wanaume 229,140 sawa na 49.7% na wanawake 232,336 sawa na 50.3%)
• Idadi ya kaya inakadiriwa kuwa 76,892 kwa wastani wa watu 6
• Ongezeko la watu kwa mwaka ni asilimia 7.1 ambapo inazidi ongezeko la Kitaifa la asilimia 3.08
Shughuli za Kiuchumi
• 85% ya wakazi hutegemea Kilimo
• Mazao makuu ya chakula ni mahindi, Mpunga, ndizi na muhogo
• Mazao ya biashara ni pamba, tumbaku, kahawa na alizeti
• 5% ya wakazi wanajishughulisha na biashara
• 8.4% ya wakazi wanajishughulisha na ufugaji
• 1.6% wameajiriwa
FURSA ZA UWEKEZAJI
1. Utalii
1.1 Hifadhi ya Taifa Burigi-Chato
• Hifadhi hii ina misitu na wanyama pori mbalimbali wa kuvutia kama vile Twiga, Tembo Nyati n.k kwa ajili ya kuona na kupiga picha
• Wilaya inamiliki eneo la jumla ya Ekari 500 katika Kijiji cha Nyabugombe Kata ya Nyakahura kwa ajili ya uwekezaji wa Hoteli za Kitalii
• Hivyo, Wilaya inakaribisha wawekezaji katika eneo la wa Hoteli za Kitalii kwa kuingia ubia na Halmashauri
• Wilaya pia inakaribisha wawekezaji katika eneo la makampuni ya kusafirisha na kuongoza watalii
1.2 Malikale
1.2.1 Pango la Bitete
• Lipo katika Kijiji cha Musenyi, Kata ya Bisibo
• Pango hili lipo chini ya miamba na lina vyumba kadhaa (Partition)
• Inasadikiwa watu kale walilitumia kufanyia maombi(mvua, ustawishaji wa mazao, kuepusha balaa n.k)
• Wilaya inakaribisha watu kufanya utalii
• Wilaya vilevile inakaribisha wawekezaji wa kufanya eneo liwe la kuvutia kwa ajili ya mapumziko (Recreation)
1.2.3 Bao kwenye Mwamba -Rwazi Lwensoro
• Hili bao lipo eneo la Kijiji cha Bisibo Kata ya Bisibo, limechimbwa kwenye mwamba.
• Yalikuwa ni makutano ya Chifu wa Biharamulo (Chifu Kasusura) na Chifu wa Karagwe (Chifu Rumanyika).
• Walikuwa wakijadili mambo ya kiutawala huku wakicheza bao
• Wilaya inakaribisha watu kufika kwa ajili ya utalii na kujifunza
1.2.4 Ikulu ya Watawala wa Jadi Biharamulo
• Ipo katika kijiji cha Nyarubungo Kata ya Nyarubungo.
• Ilijengwa mwaka 1932.
• Machifu waliotawala Biharamulo walikuwa;
1. Chifu Kasusura (Rusimbya) alitawala1887-1928
2. Chifu Ntare (Ndamugoba) alitawala1928-1958.
3 . Chifu Mankorongo II (Beelwa) alitawala1958-1960.
4. Chifu Rugaba (Stanslaus Rwanyabuswagira) alitawala1960-1964. Mbunge wa kwanza Biharamulo ambaye pia alikuwa Naibu Spika wa kwanza katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Wilaya inakaribisha watalii kwa ajili ya kujifunza mambo ya kale
1.2.5 Baadhi ya Silaha na zana zilizotumiwa na Machifu
• Baadhi ya Silaha na zana zilizotumiwa na Chifu kwa ajili ya kujilinda na wakati mwingine kuwindia wanayama ni:
• Mkuki,Upinde na kifaa cha kuifadhia mishale (Kilimba)
1.2.6 Mahakama ya Jadi (Lukiko)
• Jengo hili lilikuwa ni mahakama iliyotumiwa na Machifu.
• Lilijengwa mwaka 1932.
• Wilaya inawakaribisha watu kwa ajili ya utalii pamoja na kuwekeza katika huduma za kupumzikia (Recreation)
1.2.7 Makaburi ya Wabeligiji Walimozikwa- Vita ya II Dunia
• Makaburi hayo yapo Katika Kata ya Nyamigogo-Kijiji cha Nyamigogo na kila kaburi walizikwa askali wengi
• Tukio hilo lilitokea wakati wa vita ya pili ya Dunia.
• Pembeni mwa makaburi kuna mabaki ya Ngome ya Wajerumani
• Wilaya inawakaribisha watu kwa ajili ya utalii pamoja na kuwekeza katika huduma za kupumzikia (Recreation)
1.3 NGOMA ZA ASILI
1.3.1 Ngoma za kabila la Wasubi
•Ngoma za asili za kabila la Wasubi ni Kasimbo na Mulekule.
•Ngoma hizi huchezwa baada ya mavuno na wakati wa sherehe mbalimbali.
1.3.1 VYAKULA VYA ASILI
Vyakula vya asili vilikuwa ni:-
i. Mtama
ii.Ulezi
iii.Muhogo na
iv.Viazi
Vyakula hivyo huandaliwa kwa kutwangwa kwa kutumia kinu cha asili au kusagwa kwa kutumia jiwe (Orubengo) na kusongwa ugali
2. UWEKEZAJI KATIKA SEKTA YA MISITU
2.1 UFUGAJI WA NYUKI
• Uwepo wa mapori mengi ya hifadhi za misitu takribani Kilometa za mraba1,661
• Wilaya inawakaribisha wawekezaji wa Viwanda vya Usindikaji wa mazao ya nyuki na pia vifaa vya uvunaji wa asali
3. UWEKEZAJI KATIKA VIWANDA NA BIASHARA
3.1 Eneo la Uwekezaji Nyakanazi
• Jumla ya Hekta 10 zimetengwa kwa ajili ya uwekezaji Nyakanazi
• Halmashauri inaweka miundombinu ya maegesho ya Magari, Stendi ya Mabasi ,jengo la Biashara, huduma za maji, huduma taka ngumu na umeme ili kuvutia uwekezaji
• Wilaya inakaribisha wawekezaji kuingia ubia na Halmashauri kwa ajili ya ujenzi wa maduka makubwa, vituo vya mafuta, majengo ya ofisi za taasisi, Mabenki, Mahoteli n.k
• Eneo hili ni njia panda ya barabara za kimataifa za kwenda Burundi, Rwanda, DR Congo na Uganda
3.2 Soko la Kimkakati_ Lusahunga
• Jumla ya Ekari 61.8 zimetegwa kwa ajili ya soko la kimkakati.
• Halmashauri inataraji kujenga maghala makubwa ya kuhifadhia mazao
• Wilaya inakaribisha wawekezaji kwa ajili ya kujenga viwanda vya kuchakata mazao ya kilimo, Taasisi za umma, na maduka ma kubwa
4.1 UWEKEZAJI KATIKA SEKTA YA MADINI
Uwepo wa madini ya dhahabu
• Uchimbaji unaendelea katika mgodi wa dhahabu STAMIGOLD katika kijiji cha Mavota
• Uchimbaji mdogo wa dhahabu unaendelea katika maeneo ya Midaho, Busiri,Kumsali, Kalukwete na Msekwa
UTAFITI- Uwekezaji unaohitajika ni makampuni ya kufanya utafiti wa madini
MITAMBO YA KUCHIMBA MADINI-Kuwekeza Mitambo mikubwa ya uchimbaji na uchenjuaji wa madini
4.2 SOKO LA DHAHABU
• Soko la madini-Lusahunga limeanzishwa kwa lengo la kusogeza huduma ya kuuza na kununua dhahabu.
5. KILIMO NA MIFUGO
5.1 PAMBA
• Wilaya ya Biharamulo inazalisha Pamba kwa wastani wa Tani 347.22 kwa mwaka.
• Wilaya inakaribisha ujenzi wa maghala ya kuhifadhia Pamba.
• Wilaya inakaribisha ujenzi wa viwanda vya kuchambua Pamba na kusindika mafuta ya Pamba na chakula cha mifugo.
• Wilaya inakaribisha wawekezaji wakubwa wa zao la Pamba.
5.2 KAHAWA
• Wilaya ya Biharamulo inazalisha Kahawa kwa wastani wa Tani 128.4 kwa mwaka.
• Wilaya inakaribisha ujenzi wa maghala ya kuhifadhia Kahawa.
• Wilaya inakaribisha ujenzi wa viwanda vya kukoboa na kusindika Kahawa kwa ajili ya matumizi ya binadamu.
5.3 ALIZETI
• Wilaya ya Biharamulo inazalisha Alizeti kwa wastani wa Tani 168.7 kwa mwaka.
• Wilaya inakaribisha wawekezaji wakubwa wa zao la Alizeti.
5.5 MAZAO YA CHAKULA
MAHINDI- Wilaya ya Biharamulo inazalisha Mahindi kwa wastani wa Tani 29,822 kwa mwaka.
MUHOGO- Inazalisha Muhogo kwa wastani wa Tani 388,315.3 kwa mwaka.
NDIZI- Inazalisha Ndizi kwa wastani wa Tani 37,820.3 kwa mwaka
Wilaya inakaribisha ujenzi wa viwanda vya kutengeneza vifungashio vya kubebea mazao.
5.6 MIFUGO
NG’OMBE- Wilaya ya Biharamulo ina idadi ya Ng’ombe 132,000
MBUZI- Ina idadi ya Mbuzi 63,000
Wilaya inakaribisha ujenzi wa viwanda vya kusindika nyama, ngozi na maziwa kwa ajili ya matumizi ya binadamu.
Mtaa wa Bomani
Sanduku la Barua: S.L.P 70
Telephone: 028 2223403
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@biharamulodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya Biharamulo. Haki zote zimehifadhiwa