IDARA YA ELIMU SEKONDARI NA MAJUKUMU YAKE
Kuwakilisha Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na katika ngazi zote kuhusu masuala ya Elimu Sekondari
Kufafanua na kusimamia utekelezaji wa sera ya Elimu na mafunzo ya ufundi, sheria na kanuni zinnazoongoza utoaji wa elimu ya Sekondari
Kumshauri Mkurugenzi wa Halmashauri kuhusu masuala ya Elimu Sekondari
Kusimamia upanuzi wa elimu Sekondari katika Halmashauri
Kusimamia haki na maslahi ya walimu na watumishi wengine wa ngazi ya Elimu ya Sekondari katika Halmashauri
Kusimamia na kudhibiti akaunti ya Elimu Sekondari zinatumika kama ilivyokusudiwa
Kutayarisha na kusimamia utekelezaji wa mipango ya maendeleo ysa elimu Sekondari kila mwaka
Kufuatilia na kutathimini maendeleo ya elimu ya Sekondari katika Halmashauri,Kuhimiza shule zote za Sekondari kuinua ubora wa mazingira ya kujifunzia na kufundisha ikiwa ni pamoja na kujenga madarasa, nyumba za walimu na vyoo
Kuhimiza udhibiti wa nidhamu ya walimu na wanafunzi wa shule za Sekondari katika Halmashauri
Kufuatilia utekelezaji wa taarifa za ukaguzi wa shule za Sekondari katika Halmashauri
Kusimamia maendeleo ya taaluma na michezo ya shule za Sekondari katika Halmashauri
Kuratibu, Kukusanya na kuchambua takwimu za elimu ya Sekondari katika Halmashauri
Kuhakikisha walimu wa shule za Sekondari wanapangwa katika Halmashauri kwa kuzingatia ikama inayokubalika
Kufanya kazi nyingine kama inavyoagizwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri.=
Kuratibu na kusimamia mitihani ya Kitaifa inayoendeshwa kwa kwa shule za Sekondari katika Halmashauri
Idadi ya shule Wilaya ya Biharamulo ina shule 21 za Sekondari,kati ya shule hizo shule 19 ni za Serikali na shule 2 za dhehebu la dini,kati ya shule 19 za Serikali shule moja bado haijasajiliwa,Aidha kuna shule 5 zenye A level ambazo ni Kagango yenye michepuo ya Sayansi na sanaa,Biharamulo yenye mchepuo wa sayansi,Nyakahura yenye mchepuo wa sanaa,Mubaba yenye mchepuo wa sayansi na Nyantakala yenye mchepuo wa sayansi na sanaa.
Idara ina watumishi wa ofisini 06,wanaume 02 na wanawake 04.Katika shule za Sekondari kuna walimu 521,wanaume 326 na wanawake 195, kuna walinzi waajiriwa 02, mpishi 01 na boharia mmoja wote hawa wako katika shule ya Sekondari Kagango.Shule nyingine wanatumia vibarua ambao shule husika inawalipa mishahara.
Wilaya ina wanafunzi 9,219 wakiwemo wavulana 5071 na wasichana 4,148.Kwa shule binafsi idadi ya wanafunzi ni 666 wavulana 302 wasichana 364
Hali ya miundombinu ya Wilaya ina mahitaji ya vyumba vya madarasa 227,madarasa yaliyopo ni 224 sawa na asilimia 98.7 Mahitaji ya vyumba za walimu ni 324 nyumba zilizopo ni 70 sawa na asilimia 21.6.Mahitaji ya maktaba ni 21 na maktaba zilizopo ni 21 sawa na asilimia 9.5.
Mahitaji ya maabara ni 54 maabara zilizokamilika ni 14 sawa na asilimia 25.9.Aidha mahitaji ya Hostel ni 36 na Hosteli zilizopo ni 11 sawa na asilimia 30.5
MKUU WA IDARA JUDITH KIBONA 076424447 .
Mtaa wa Bomani
Sanduku la Barua: S.L.P 70
Telephone: 028 2223403
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@biharamulodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya Biharamulo. Haki zote zimehifadhiwa