IDARA YA ELIMU MSINGI NA MAJUKUMU YAKE
Kuwakilisha Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na katika ngazi zote
Kufafanua na kusimamia utekelezaji wa sera ya Elimu na mafunzo, sheria na kanuni katika Elimu ya Watu Wazima na ufundi stadi
Kumshauri Mkurugenzi wa Halmashauri kuhusu masuala ya Elimu
Kuthibiti matumizi ya fedha za elimu kwa mujibu wa miongozo ya fedha za Serikali
Kushughulikia upanuzi wa elimu katika ngazi ya elimu ya awali,Elimu ya Msingi,Elimu ya Sekondari na Mafunzo ya ualimu, Elimu ya watu wazima na vituo vya ufundi stadi.
Kufuatilia kwa madhumuni ya kutathmini maendeleo ya Elimu katika Wilaya
Kutayarisha na kusimamia utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya Elimu kila mwaka
Kuhakikisha kwamba shule zote zinaboresha mazingira ya kufundishia
Kuhimiza uthibiti wa nidhamu ya walimu na wanafunzi Wilayani
Kuratibu na kusimamia mitihani ya Darasa la nne,darasa la saba mafunzo ya ualimu na mitihani ya vituo vya ufundi stadi katika wilaya kwa kushirikiana na uongozi wa elimu Mkoa na Baraza la mitihani Tanzania
Kufuatilia taarifa za utekelezaji wa taarifa za ukaguzi wa shule na vyuo
Kusimamia maendeleo ya taaluma na Michezo katika Wilaya
Kukusanya, kuratibu na kuchambua takwimu za elimu katika wilaya kwa ajili ya Mipango ya Maendeleo katika ngazi ya Shule.Wlaya, Mkoa na Taifa.
Kusimamia upanuzi wa elimu Sekondari katika Halmashauri
KAIMU MKUU WA IDARA JESSY PAUL .NO, SIMU 0714118454
Mtaa wa Bomani
Sanduku la Barua: S.L.P 70
Telephone: 028 2223403
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@biharamulodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya Biharamulo. Haki zote zimehifadhiwa