Biharamulo ni mojawapo ya Wilaya nane katika Mkoa wa Kagera yenye eneo la kilometa za mraba 5,627. Kwa upande wa kaskazini Wilaya inapakana na Wilaya ya Muleba na Karagwe Kusini inapatikana Wilaya ya Bukombe na Wilaya Kakonko.Kwa upande wa magharibi inapakana na Wilaya ya Ngara na Mashairki inapakana na Wilaya ya chato.Wilaya ya Biharamulo Imegawanyika katika Tarafa mbili (2) za Nyarubungo na Lusahunga.Pia inazo Kata kumi na saba zenye jumla ya vijiji 74 na vitongoji 384.
Kwa upande wa Mashariki inapakana na Wilaya mpya ya Chato, kwa upande wa Magharibi inapakana na Wilaya ya Ngara, kwa upande wa Kaskazini Wilaya inapakana na Wilaya ya Muleba na Karagwe na Kusini inapakana na Wilaya za Bukombe na Kakonko.
Wilaya ipo kilometa 171 kutoka makao makuu ya Mkoa wa Kagera. Wilaya inapatikana kati ya nyuzi 20 15’ - 3015’ kusini mwa Ikweta na 310 - 320 Mashariki mwa “Standard Meridian”. Pia Wilaya ipo kwenye mwinuko wa kati ya mita 1135 – 1410 kutoka usawa wa bahari
Mtaa wa Bomani
Sanduku la Barua: S.L.P 70
Telephone: 028 2223403
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@biharamulodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya Biharamulo. Haki zote zimehifadhiwa