IDARA YA UTUMISHI NA UTAWALA NA MAJUKUMU YAKE
Kubaini nafasi wazi zilizopo katika Halmashauri na kuratibu ujazaji wa nafasi hizo.
Kuratibu uthibitishwaji kazini wa watumishi kwa mujibu wa ya 14(1)&(7) ya Kanuni za Utumishi wa Umma za mwaka 2003.
Kuratibu shughuli vyeo/madaraja watumishi wa Halmashauri kwa kuzingatia utendaji kazi wa watumishi, muda aliotumikia cheo/daraja alilonalo na sifa za kitaaluma alizonazo kadri ya muundo wa kada husika.
Kutunza kumbukumbu za kiutumishi za watumishi wote wa Halmashauri.
Kuhakiki mara kwa mara kumbukumbu za watumishi kwa mujibu wa kanuni ya 32(3) ya kanuni za utumishi wa Umma za mwaka 2003 kwa lengo la kubaini tarehe ya kustaafu ya kila mtumishi
Kuratibu usimamizi wa nidhani ya kazi ya watumishi na kuhakikisha kuwa hatua za kinidhamu dhidi ya watumishi zinafuata sheria na kanuni za Utumishi
Kuandaa ikama na Bajeti ya watumishi na mishahara ya kila mwaka.
Kuratinu ufanyikaji wa vikao vyote vya kisheria katika ngazi ya Halmashauri, Kata na Vijiji.
Kusimamia matumizi ya Mali za Halmashauri na kuhakikisha kuwa kumbukumbu ya mali hizi inatunzwa kadri ya matakwa ya randama ya Fedha ya Serikali za Mitaa ya mwaka 2009
Kusimamia matumizi ya magari ya Halmashauri.
Kuhakikisha kuwa upimaji wa utendaji kazi wa kila mtumishi unapimwa kwa njia ya OPRAS
Kuandaa taarifa mbalimbali za kiutumishi kwa kila robo mwaka na kuziwasilisha mamlaka husika (Kwa Katibu Tawala wa Mkoa, TAMISEMI na Tume ya Utumishi wa Umma)
Kuratibu ubainishaji wa mapungufu ya watumishi ya kiutendaji na kuaandaa mpango wa kujenga uwezo /mpango wa mafunzo
Kuhudhuria vikao vya kisheria vya Halmashauri.
MKUU WA IDARA EMILIAN R.RUGANAMULA .NO, SIMU 0783049049.
Mtaa wa Bomani
Sanduku la Barua: S.L.P 70
Telephone: 028 2223403
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@biharamulodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya Biharamulo. Haki zote zimehifadhiwa