KITENGO CHA TEKNOLOJIA, HABARI, MAWASILIANO NA UHUSIANO NA MAJUKUMU YAKE
Kitengo cha (TEHAMA) kimeanzishwa mwaka 2013 ambacho ni muunganiko wa Kitengo na Uhusiano. Kitengo hiki kinaongozwa na Sera ya TEHAMA (2003), na Sera ya Utangazaji Habari (2004). Ibara ya 18 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaeleza kuwa 1) bila ya kuathiri sheria ya nchi, na kutafuta,kupata na kueneza au kusambaza habari na mawazo kupitia chombo cha habari chochote bila ya kujali mipaka ya taifa pia anayo haki na uhuru wa kutoingiliwa na mawasiliano (2) kila raia ana haki ya kupashwa habari wakati wote kuhusu matukio mbalimbali ya nchini na duniani kote yenye umuhimu kwa maisha na shughuli za wananchi , pia kwa masuala yenye umuhimu kwa jamii.
Majukumu ya Kitengo
Kuweka mahusiano bora baina ya Halmashauri pamoja na Umma na wadau mbalimbali pamoja na kutoa elimu kwa Umma.
Kuandaa machapisho mbalimbali ya Halmashauri.
kuratibu masuala ya kiitifaki ikiwemo kupokea wageni.
Usimamizi Wa Mifumo ya Kompyuta
Usimamizi wa tovuti na barua pepe
Kutekeleza sera ya TEHAMA na Serikali Mtandao.
Kuandaa mahitaji katika Ununuzi wa vifaa vya TEHAMA.
Teknolojia ya Habari, Mawasiliano na Uhusiano (TEHAMA)
Mtaa wa Bomani
Sanduku la Barua: S.L.P 70
Telephone: 028 2223403
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@biharamulodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya Biharamulo. Haki zote zimehifadhiwa