Wananchi Wote,
TANZANIA BARA.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo anawatangazia wanachi nafasi za kazi kama ifuatavyo:-
KATIBU MAHSUSI III (nafasi moja)
Mwombaji anatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:-
i.Awe amehitimu na kufaulu Elimu ya kidato cha nne.
ii. Awe amehitimu mafunzo ya uchapaji katika ngazi ya Cheti (Astashahada)
iii. Awe na ujuzi wa kutumia Kopyuta.
Masharti ya Kazi:-
i.Kazi hii ni ya masharti ya kudumu na malipo ya uzeeni
ii.Kazi hii ina ngazi ya mshahara TGS B kwa viwango vya Serikali.
WASAIDIZI WA HESABU (nafasi 2)
Mwombaji anatakiwa awe na sifa zifuatazo:-
i.Awe amehitimu kidato cha (iv) au (vi)
ii. Awe na Astashahada ya Uhasibu kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
Masharti ya Kazi:-
i.Kazi hii ni ya mkataba wa miaka miwili na mkataba huu waweza kuuhishwa
ii.Kazi hii ina ngazi ya mshahara TGS B kwa viwango vya Serikali.
MASHARTI YA JUMLA.
Mwombaji anatakiwa kuambatisha:-
i.Nakala za vyeti vya mafunzo
ii.Maelezo binafsi (Curriculum Vitae)
iii.Picha ndogo za rangi mbili (2) za mwombaji za hivi karibuni.
iv.Cheti cha kuzaliwa.
N.B. Maombi yote yatumwe kupitia posta kwa anuani ya Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya S.L.P 70, Biharamulo.
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 30/6/2019 saa 9:30 alasiri
Wende I. Ng’ahala
MKURUGENZI MTENDAJI (W)
BIHARAMULO
Mtaa wa Bomani
Sanduku la Barua: S.L.P 70
Telephone: 028 2223403
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@biharamulodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya Biharamulo. Haki zote zimehifadhiwa