HALMASHAURI YA WILAYA YA BIHARAMULO
Wananchi Wote,
HALMASHAURI YA WILAYA.
BIHARAMULO.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo anawatangazia wanachi kujaza nafasi wazi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ajira ya Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo kutuma maombi yao.
SIFA ZA MWOMBAJI:-
KAZI ZA MWENYEKITI WA BODI:-
Ataitisha na kuendesha vikao vya kila robo ya mwaka na vya dharura vya Bodi ya Ajira ya Halmashuri ambavyo hushughulikia masuala ya Ajira. Upandishaji vyeo, ubadilishaji muundo na uthibitishwaji kazini watumishi.
KIPINDI CHA KUDUMU OFISINI.
Uenyekiti wa Bodi ya Ajira si kazi ya ajira yenye mshahara na inadumu kwa muda wa miaka mitano sawa na ujumbe wa Baraza la Madiwani.
Endapo kipindi cha Mamlaka ya Halmashauri kitaisha kabla ya kipindi cha miaka mitano ya Uenyekiti wa Bodi ya Ajira, ikimalizika Uenyekiti huu utasimama hadi Mamlaka ya Halmashauri itakaporejea tena.
MASLAHI YA UENYEKITI.
Mwenyekiti wa Bodi ya Ajira halipwi mshahara isipokuwa wakati wa kuendesha vikao atalipwa nauli na posho ya kikao kwa viwango vya Serikali vilivyopo.
MUDA WA MAOMBI.
Kwa yoyote mzalendo na mwenye sifa zilizotajwa hapo juu mwenye nia ya kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ajira ya Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo atume maombi yake kwa njia ya posta akielekeza kwa :-
Mkurugenzi Mtendaji (W),
S.L.P 70,
BIHARAMULO.
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 22/07/2019 Saa 9:30 alasiri
Wende I. Ng’ahala
MKURUGENZI MTENDAJI (W)
BIHARAMULO
Mtaa wa Bomani
Sanduku la Barua: S.L.P 70
Telephone: 028 2223403
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@biharamulodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya Biharamulo. Haki zote zimehifadhiwa