Tarehe 29/11/2017 majira ya saa sita mchana, mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali na mawe ilinyesha katika Kata tajwa hapo juu na kusababisha nyumba kadhaa kuezuliwa na mazao mashambani kuharibiwa.
Aidha hakukutokea majeruhi wala vifo vilivyotokana na maafa kwenye maeneo hayo.
MADHARA YALIYOTOKEA KWENYE MAAFA HAYO
Jumla ya nyumba 14 ziliharibiwa katika viwango mbalimbali, hasa kuezuliwa kwa mapaa.
Hakuna vifo wala majeruhi na angalau waathirika wote wana mahali wanapojihifadhi katika vyumba ambavyo havijaathirika katika maeneo yao na waathirika wao wenyewe na kwa kusaidiwa na majirani wanafanya jitihada za kuezeka mapaa yaliyoezuliwa.
Jumla ya nyumba 34 katika kijiji cha Ruziba, Kata ya Ruziba yenye vijiji 4 na kijiji pekee kilichoathiriwa na maafa hayo katika Kata hiyo. Kijiji hicho chenye Jumla ya kaya 560 pia kimeathirika kati kilimo ,kwani jumla ya ekari 142.5 zimeharibiw katika viwango tofauti. Athari katika mazao ni kama ifuatavyo:-
Migomba ekari 56
Mahindi ekari 54
Maharage ekari 29
Mazao ya bustani ekari 2.5
Jumla ni ekari 142.5.
TATHMINI YA AWALI ILIYOFANYWA NA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA NA KAMATI YA MAAFA YA WILAYA
Baada ya Kamati tajwa hapo juu kushuhudia maafa hayo katika maeneo yaliyoathiriwa ilibaini mambo yafuatayo kama ndio yaliyochochea maafa hayo kuwa makubwa:-
Nyumba nyingi zilizoezuliwa ni zile zilizochakaa (zenye umri mkubwa) na na ambazo hazikuezekwa kwa mujibu wa taratibu za kiufundi.
Hakuna majeruhi wala vifo vilivyotokea katika maafa haya.
Nyumba za taasisi zilizoezuliwa ni jingo la Jeshi la Akiba (Mgambo) mjini Biharamulo.
Mazao yameharibiwa na mawe na upepo mkali mfano migomba, mahindi, maharage na mazao ya bustani. Aidha zao la mahindi halitaathirika sana kwani tunatarajia yatakua vizuri kwani mengi yako katika hatua za awali z ukuaji. Maharage na mazao ya bustani yameharibika kwa kiwango cha wastani. Migomba mingi iliyoharibika haitovunwa hadi vichipukizi vitakapokuwa ingawa haiwezi kusababisha uksefu wa chakula kwa waathirika.
MAELEKEZO NA USHAURI WA KAMATI
Wananchi washauriwe kufanya ujenzi wa nyumba kwa kufuata utaalamu ili kuepuka kutokea kwa ajali zisizokuwa za lazima.
Majirani, ndugu jamaa na marafiki wawasaidie waathirika kuweza kuezeka upya nyumba zao na kuwasaidia sehemu za kulala wakati wakipaua nyumba zao.
Halmashauri ya wilaya ifanye jitihada haraka za kupaua nyumba ya mwalimu iliyoezuliwa ili mwalimu aendelee kuishi maeneo ya shule.
Nyumba ya Jeshi la Mgambo itakarabatiwa na wahusika na kwa muda wahamishie shughuli zao kwenye majengo mengine waliyoyajenga.
Wananchi washauriwe kupanda miti kwenye makazi yao ili kukinga upepo usiezue nyumba zao, kwani nyumb zote zilizokwenye miti katika maeneo yaliyoathirika hazikuezuliwa.
Katika maafa haya hakuna muathirika ambaye maafa haya yamesababisha upungufu/ukosefu wa chakula kwa sasa.
Cornel P. Mwasote
Mratibu wa Maafa (w),
BIHARAMULO.
Mtaa wa Bomani
Sanduku la Barua: S.L.P 70
Telephone: 028 2223403
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@biharamulodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya Biharamulo. Haki zote zimehifadhiwa