Kwamba Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Biharamulo anawatangazia wananchi wote na wadau wa maendeleo ya kuendeleza ardhi na upendezeshaji wa miji yetu ya Biharamulo, kuwa Halmashauri ya Wilaya ilipima na sasa inauza viwanja vyake katika maeneo matatu(3) ya Nyakanazi( Uwekezaji maarufu kama eneo la Parking ya malori makubwa), Lusahunga( Chema/Mnada wa Ng’ombe) na Kabindi ( Chebitoke), ambavyo viko katika matumizi mbalimbali kama ifuatavyo:-
1. ENEO LA NYAKANAZI
Viwanja hivi ni kwa ajili ya uwekezaji wa Majengo ya Biashra ya aina mbalimbali kuanzia Mahoteli makubwa, Benki na shughuli za kifedha, maduka makubwa ya super market n.k. Viwanja vinapatika mkabala na eneo la uwekezaji wa Maegesho ya malori makubwa ya mizigo barabara kuu ya kuelekea Kahama kutokea junction ya Nyakanazi mkono wa Kushoto kwenda kahama. Eneo hili mbali na kujengwa maegesho ya malori pia litajengwa stendi kubwa ya mabasi ya Nyakanazi ambayo itajengwa mbele ya kituo cha Polisi junction ya Nyakanazi. Viwanja hivi pia vinatazaman na Kituo kukubwa cha Mafuta cha Ngara Oil na Hoteli mpya ya Ruhinda. Huduma ya maji ,umeme na nyinginezo muhimu itawekwa kwa ajili ya kurahisisha ujenzi wa Majengo ya kisasa.
Viwanja hivi vinapatika kwa bei ya Tshs. 12,000/= kwa mita ya mraba , fedha hii ikijumuisha malipo yote ikiwa ni pamoja na mnunuzi kupatiwa hati ya miaka 99.
2. ENEO LA LUSAHUNGA
Viwanja hivi vinapatika katika eneo la Halmashauri malufu kama kituo cha kilimo ilipo ofisi ya kata Lusahunga. Viwanja hivi vimetazamana na eneo la mnada wa Ng’ombe wa Alhamisi. Eneo linapakana na eneo la kanisa katoliki maarufu kama kama eneo la CHEMA.
Viwanja hivi ziko katika matumizi mbalimbali wa makazi, biashara na makazi pamoja na ujenzi wa maghara makubwa ya mizigo na mashine za kungeza thamani ya mazao.
Viwanja vinapatikana kwa bei ya Tshs. 1,200/= kwa viwanja vya makazi kwa mita ya mraba, Tshs 1,500 = kwa viwanja vya makazi na biashara na Tshs. 3,000/= kwa viwanja vya ujenzi wa maghara ya kuhifadhia mizigo
3. ENEO LA KABINDI
Kwa upande wa kabindiKabindi - Chebitoke viwanja hivi vinapatikana katika eneo kilipojengwa kituo cha Mafuta cha Kanisa Katoliki jimbo la Rulenge –Ngara, upande wa juu wa kituo. Ni mkono wa kulia kutoke shule ya sekondari Rwagati kuelekea kabindi Center( Kitovu cha Mji wa Kabindi). Katika eneo hili ndiko kuliko pangwa kujengwa Stendi kubwa ya mabasi ya Kabindi.
Huduma ya umeme na maji viko ndani ya eneo husika. Pia mbali na viwanja vya kawaida pia kuna kiwanja cha kuabudia ambacho nacho kinauzwa.Viwanja vinapatika kwa bei ya Tshs. 1,200/= kwa mita ya mraba.
4. UTARATIBU WA UPATIKANAJI VIWANJA.
(a) Mhitaji anatakiwa kufika ofisi ya ardhi kwa ajili ya kupata maelezo ya ziada kwa kuangalia michoro ya viwanja na kuchagua kiwanja anachotaka.
(b) Mhitaji baada ya kuchagua kiwanja atajulishwa bei yake kulingana na matumzi na ukubwa wa kiwanja husika alicho chagua.
(c) Mhitaji atalazimika kulipa ada ya maombi Tshs 20,000/= ambayo haitarudishwa akishnindwa kulipia malipo ya kiwanja.
(d) Mhitaji atalazimika kulipia malipo ya awali kulingana na jinsi malipo yatakavyokuwa kwa maana malipo haya yanatakiwa kulipwa ndani ya miezi sita tangu ulipochangua kiwanja kwa utaratibu utakaoweka kati ya mlipaji na ofisi ya mkurugenzi.
(e) Malipo haya yanaweza kulipwa kwa awamu sita au mara moja au vinginevyo ndani ya miezi zita kulingana na makubaliano ya kiofisi.
5. MAHITAJI YA VIELELEZO
Mwombaji anatakiwa awe na kitambulisho ha NIDA au cha Mpiga kura , au Leseni ay Udereva au Pass ya kusafiria ya Kudumu au Cheti za uraia. Kwa Taasisi au makampuni mwambaji anatakiwa awe na nyaraka za usajiri wa taasisi na viatmbulisho vya wakurugenzi wa kampuni au Taasisi. Pamoaja na nyaraka nyinginezo kadri atakavyojulishwa na Afisa Ardhi ambavyo vinampa au vinaipa sifa taasisi au kampuni au kikundi mkumiliki ardhi ndani ya nchi ya Tanzania.
6. MWISHO
Kwa wale ambao watakuwa nje ya Biharamulo na wanahitaji kupata maelezo ya ziada wawasiliane na Ofisi ya Mkurugenzi moja kwa moja au kupitia Idara ya Ardhi kwa ajili ya kujibiwa maswali au mahitaji yao.
WANANCHI NA WADAU NYOTE MNAKARIBISHWA.
Dkt. Sospeter B. Mashamba
KAIMU MKURUGENZI MTENDAJI (W)
BIHARAMULO
Mtaa wa Bomani
Sanduku la Barua: S.L.P 70
Telephone: 028 2223403
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@biharamulodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya Biharamulo. Haki zote zimehifadhiwa