Afisa Biashara wa Wilaya ya Biharamulo Mkoa wa Kagera, Bahati Dominick amesema vitambulisho vya wajasiliamali wadogo vimetolewa kwa wachache waliohakikiwa ambao hawajahakikiwa ni wengi na wako vijiji hivyo kuwataka watendaji wa kata na vijiji kuwahamasisha wananchi juu ya umuhimu wa kuwa na vitambulisho vya wajasiliamali wadogo wadodo ili kufanya biashara zao katika maeneo mbalimbali bila usumbufu.
Dominick ameyasema hayo wakati akitoa taarifa kwa Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo Kanali Mathias Kahabi ,ambaye amewakilishwa na Mwenyekiti wa Halmashuri ya Biharamulo Leo Rushahu kwenye hafla ya uzinduzi wa vitambulisho vya wajasiliamali ambayo imefanyika katika ukumbi wa Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo May 4, 2021.
Amesema mwaka 2019 walipokea vitambulisho 7770 na kuviuza ambapo mwaka 2020 walipokea vitambulisho 8600 kati ya hivyo vilivyouzwa 5774 na mwaka huu 2021 wamepokea vitambulisho 8200 ambavyo vimeuzwa ni vitambulisho 203 ila walivyo vikabidhi leo ni 83 ambavyo vimehakikiwa.
“Wajasiliamali ambao hawatahusika na kugawiwa vitambulisho nipamoja na mafundi welding, wanahusika na uchomeleaji wa vyuma, saluni kubwa, na wale wafanya biashara wakubwa wenye leseni”, Amesisitiza Dominick.
Dominick ameogeza kuwa kutakuwa na msako wa kukagua wajasiliamali wenye vitambulisho kabla hawajaingia sokoni, kwa wale ambao watakutwa hawana hawataruhusiwa kuingia sokoni hii itawasaidia kuepusha mgogoro kwa wale waliolipia.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Biharamulo, Leo Lushahu aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo Kanali Matias Kahabi amesema wajasiliamali wakilipia vitambulisho vya Tsh 20,000 elfu watapa haueni ya kulipa Tsh 1,000 elfu kila wanapo ingia sokoni ambapo kwa mwaka itakuwa zaidi laki moja.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo Dr Sospiter Mashamba, amewaomba wajasiliamali kuwa mabarozi wazuri kwa wengine ili nao waweze kunufaika na vitambulisho vilivyoboreshwa.
Akizungumza kwa niaba ya Madiwani wa Halmashauri ,Diwani wa Kata ya Biharamulo Mjini Devidi Mwenenkundwa amewaomba viongozi watakaohusika na zoezi la kukagua vitambulisho kutowasumbua wajasiliamali ambao wanakamilisha taratibu za kupata vitambulisho hivyo.
Nae mjasiliamali wa Soko la Kasusula Biharamulo Mjini, Levina Jeremiah, amesema anaishukuru sana Serikali kwa kuleta vitambulisho vya wajasiliamali maana vimekuwa neema kubwa kwao kwa kufanya biashara kwa uhuru bila kusumbuliwa.
Imeandikwa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo
Mtaa wa Bomani
Sanduku la Barua: S.L.P 70
Telephone: 028 2223403
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@biharamulodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya Biharamulo. Haki zote zimehifadhiwa