Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo MkoaNI Kagera, Waziri K. Kombo, awasisitiza Madiwani kuweka usimamizi mzuri kwa wananchi wanaogawiwa ardhi wanauze horela bila utaratibu maalumu wa kisheria.
Ameyasema hayo wakati wa Baraza la Madiwani la kuwasilisha taarifa za kila kata lililofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo 29/4/2021.
Amewasisitiza Madiwani kufatiria taarifa vizuri za watoto kuchelewa kuripoti shuleni kwa wakati ambao wanahitajika kufika na tatizo la wanafunzi wanaopewa mimba bila kufatiria wahusika wanao wapa mimba, hilo ni jukumu lenu kuhakikisha mnalifanyia kazi.
“ Afisa Elimu wa Halmashauri afatirie wanafunzi takiribani asilimia 18.5 ambao hawajaripoti shuleni na alete taarifa zao kamili”, Amesema Kombo.
Kombo amemuomba Diwani wa Kata ya Ruziba kumsimamia Mtendaji wake katika makusanyo ya PoS yaliyoonekana kuwa sio mazuri.
Hata hivyo ametoa shukurani zake za dhati kwa Madiwani wote waliohudhuria Baraza hilo la kuwasilisha taarifa za Kata amekubari kupokea changamoto zilizojitokeza na ushauri uliotolewa pamoja na kuhaidi kuzifanyia kazi.
Imeandaliwa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo
Mtaa wa Bomani
Sanduku la Barua: S.L.P 70
Telephone: 028 2223403
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@biharamulodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya Biharamulo. Haki zote zimehifadhiwa