Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo Mkoa wa Kagera, Kanali Mathias Kahabi aipongeza menejimenti ya Halmashauri hiyo kwa usimamizi mzuri wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Biharamulo ambao upo hatua nzuri inayolidhisha.
Pongezi hizo amezitoa wakati alipofanya ziara fupi ya kushitukiza leo May 7, mwaka huu katika eneo la Katoke kata ya Nyarubungo inapojengwa hospitali hiyo.
Vilevile, amempongenza msimamizi wa mradi huo, mhandisi Imani Kibona kwa ubunifu alioufanya wa kuweka kila jengo fundi Mkuu mmoja jambo ambalo limesaidia ujenzi huo kwenda kwa kasi.
“Mhandisi naomba uongeze nguvu ya usimamizi kwenye majengo ambayo hayajaezekwa ili nitakaporudi kwa mara nyingine nikute kuna mabadiliko”, Amesema Kahabi.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, hiyo Waziri K. Kombo amesema kulikuwa na changamoto ya maji iliyotokana na umeme kusumbua lakini mpaka sasa imeshatatuliwa, kwahiyo amewataka mafundi wafanye kazi kwa bidii ili waweze kumaliza mradi huo kwa wakati.
Imeandaliwa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo.
Mtaa wa Bomani
Sanduku la Barua: S.L.P 70
Telephone: 028 2223403
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@biharamulodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya Biharamulo. Haki zote zimehifadhiwa