Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo Mkoa wa Kagera Kanali Mathias Kahabi awahakikishia Wananchi na Waislamu wote kwamba Vyombo vya Ulinzi na Usalama vimejipanga vizuri kuhakikisha wanasherehekea Sikukuu ya Eid katika hali ya utulivu na Amani.
Ameyasema hayo leo may 12, 2021 ofisini kwake wakati akitoa taarifa fupi ya hali ya Ulinzi na Usalama kuelekea Sikukuu ya Eid El Fitri.
Kahabi anawasisitiza Wananchi wasiwe na hofu viongonzi wote wa Vyombo vya ulinzi na Usalama wamejipanga vema kuhakikisha Usalama unaimalishwa katika kipindi chote cha Sikukuu na baada ya Sikukuu. Pia anawaomba viongozi wote wa Serikali, viongozi wa Dini pamoja na Wananchi, mtu yeyote atakayepata taarifa za mipango yoyote ya kihalifu asisite kutoa taarifa kwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama.
Vilevile amesemma Serikali inatambua umuhimu mkubwa wa viongozi wa Dini hasa katika kudumisha Amani kwenye Taifa latu. Tunaendelea kuwaomba viongozi wa Dini msichoke kuhubiri Amani, Upendo na utulivu katika nchi yetu ya Tanzania.
“Nawasihi wazazi wote wa Wilaya ya Biharamulo kuwa waangalifu zaidi kwa watoto wasiwaache peke yao katika kipindi cha Sikukuu ya Eid El Fitri bila uangalizi wa watu wazima ili kuepusha matatizo kama ya ajali na matukio ya kupotea”, Amesisitiza Kahabi.
Hatavyo, anaomba kuwatakia Sikukuu njema ya Eid El Fitri Waislamu na Wananchi wote wa Wilaya ya Biharamulo. Pia ametoa rai kwamba wayaendeleze yale mema yote waliyoyapata wakati wa mfungo wa Mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Imeandaliwa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo
Mtaa wa Bomani
Sanduku la Barua: S.L.P 70
Telephone: 028 2223403
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@biharamulodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya Biharamulo. Haki zote zimehifadhiwa