Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo Mkoa wa Kagera, Kanali Mathias Kahabi amewaagiza viongozi wa vijiji kusimamia ulinzi na usalama katika maeneo yao husika ili kuweza kuondoa muingiliano wa raia wa kigeni wanaoingia nchini bila utaratibu maalumu.
Ameyasema hayo katika ukumbi wa shule ya msingi Biharamulo 13/04/2021 wakati akitoa mafunzo kazi kwa viongozi wa ngazi ya kata, vijiji na tarafa jinsi ya kuzitatua na kuzipokea kero za wananchi.
Amewataka viongozi wote kutumia vizuri dhamana ambayo wamepewa na serikali katika majukumu yao ,kwa kutumia kauli nzuri na busara wakati wa kutatua kero na changamoto ambazo wanapokea kutoka kwa wananchi pia kuonesha upendo na ushirikiano ili kuweza kuondoa uvunjifu wa amani katika jamii.
“Kila siku ya jumanne ofisi zote za watendaji wa vijiji wanatakiwa kupokea na kutatua kero za wananchi ili kuondoa migogororo ambayo inaweza kuleta uvunjifu wa amani kwa jamii”, amesema Kahabi.
Pia Kahabi amewataka watendaji wa vijiji na kata kila baada ya miezi mitatu kufanya mikutano ya kisheria na wananchi ili kujua kero zao na kuzitatua,
Nae, Kamanda wa TAKUKURU Wilaya ya Biharamulo Siaba Ilumbo, amewaagiza watendaji wote wa kata na vijiji kuacha tamaa za kupokea na kuomba ruswa hali ambayo inawanyima haki wananchi wanyonge.
Kwa upande wake kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo Dr Sospiter Mashamba amesema watendaji wanatakiwa kutumia busara wakati wanapokusanya mapato ya Serikali.
Mwenyekiti wa kijiji cha Rusenga kata ya Kalenge Paskali Mbungani, amesema wapo tayari kuzipokea na kuzitatua kero na changamoto mbalimbali za wananchi ambazo zinapelekea uvunjifu wa amani katika jamii.
Imeandaliwa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo
Mtaa wa Bomani
Sanduku la Barua: S.L.P 70
Telephone: 028 2223403
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@biharamulodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya Biharamulo. Haki zote zimehifadhiwa