Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2022, Ndg. Sahili Nyanzabara Geraruma amewasihi wakazi wa Wilaya ya
Biharamulo kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassankwa kuunganisha huduma ya maji katika nyumba zao na hii ndio
itakuwa maana halisi ya kumtua mama ndoo kichwani.
Akizungumuza na wananchi leo mara baada ya kuzindua mradi wa maji Ruganzu, uliopo Kata ya Nyanza, Wilaya ya Bihalamulo wenye thamani ya shilingi milioni 114.3
Mwenge wa Uhuru umezindua Mradi wa Maji Ruganzu na vyumba viwili vya madarasa Shule ya Wasichana Kagango kwa fedha za UVICO-19
Miradi miwili imewekwa jiwe la msingi ambayo ni Mradi wa barabara ya lami, Rukaragata-Kibamba kilometa moja na Kituo cha Afya cha Bisibo kwa fedha za Tozo.
Sambamba na kukagua shughuli za lishe, umekagua mapambano dhidi ya malaria,mapambano ya dawa za kulevya na kuzindua klabu ya wapinga rushwa shule ya Sekondari Nyakanazi.
Aidha, Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa amewataka wataalam wanaosimamia miradi ya Serikali kuhakikisha wanafuata taratibu na maelekezo ya
matumizi ya fedha kama vile miongozoinavyowaelekeza ili miradi iwe yenye tija na yenye manufaa kwa wananchi.
Mwenge wa Uhuru umepokelewa leo tarehe Oktoba 6,2022 Mkoani Kagera utakagua, kutembelea na kuzindua jumla ya miradi 37 yenye thamani ya shilingi bilioni 13.6 katika sekta za Afya, Elimu, Maji, Barabara na miradi ya watu binafsi kwaHalmashauri nane.
Mtaa wa Bomani
Sanduku la Barua: S.L.P 70
Telephone: 028 2223403
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@biharamulodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya Biharamulo. Haki zote zimehifadhiwa