Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo Mkoa wa Kagera, Leo Lushahu awaomba wananchi wa kata ya Kabindi wasiogope kuwekeza katika stendi hiyo ili kuweza kukuza uchumi wa mji huo pia amewahakikishia ulinzi na usalama wa mali zao .
Ameyasema hayo baada ya uzinduzi wa stendi mpya ya mabasi katika kijiji cha Kikomakoma kata ya Kabindi June, 4, 2021.
Lushahu, awasihi Vijana wa bodaboda kuchangamkia fursa ya kujiali katika stendi hiyo mpya kwa kuzingatia kanuni na taratibu zilizowekwa na sheria ya usalama barabarani.
“Tumejipanga kuhakikisha tunaboresha stendi hii kwa kiwango cha juu zaidi kutokana na ushirikiano wenu katika uwekezaji”, amesisitiza Lushahu.
Afisa Biashara wa Wilaya ya Biharamulo Mkoa wa Kagera, Bahati Dominick amesema wanakusudia kuingiza magari takribani 150 kwa siku kwa ajili ya usafiri. Stendi hii ni mojawapo ya chanzo cha mapato ya Halmashauri ikiwa ni pamoja na kukuza uchumi wa Halmashauri.
Dominick amesema kutakuwa na utaratibu wa kutoza ushuru kwa kila gari linalo ingia stendi kwa ajili ya kusafirisha abiria kama sehem zingine kwa gharama zifutazo Basi kubwa Tshs 3000 Tax Tshs 1000 Mini Bas Tshs 2000 na Costa Tshs 3000 Tunatarajia kukusanya mapato kupitia stendi hiyo kwa mwaka zaidi ya Tshs milioni 54,000,000.
Vilevile ameongezea kwamba wanatalajia kuanza kukusanya mapato ya Halmashauri 7/6/2021 pia anawaomba wananchi waweze kutoa ushirikiano ili waweze kuongeza mapato ya Halmashauri.
Kwa upande wake diwani wa kata ya Biharamulo mjini Devidi Mwenenkundwa amewaomba wananchi wa kata ya kabindi kuiunga serikali mkono kwa ajiri ya kuinua uchumi wa Halmashauri pia kuwataka waache siasa wafanye kazi ya kimaendeleo katika stendi hiyo.
Afisa usalama barabarani kata ya Kabindi Magoma Peter, amewahakikishi wananchi wa kata ya Kabindi kwamba wamejipanga vizuri kuhakikisha wanazuia ajari katika eneo la stendi na atakae bainika anavunja sheria ya usalama barabarani hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.
Nae, Mwenyekiti wa wawekezaji Kikomakoma kata ya Kabindi Goderiva Binamungu amesema wawekezaji walifanikiwa kujenga vibanda kwa muitikio mkubwa ambapo vibanda 80 vimejengwa, kulipia kwa 100% eneo la wawekezaji, ushirikiano wa wawekezaji na afisa mtendaji wa kijiji.
Hatahivyo amezitaja changamoto mbalimbali zinazowakwamisha katika shughuli zao uhaba wa fedha za kumalizia ujenzi, wizi wa mali za wawekezaji mfano kuibiwa fremu za milango, mtazamo hasi wa jamii juu ya mradi wa soko na stendi.
Binamungu, ameyasema matarajio ya mradi wa stendi hiyo ni kuongeze kipato kwa wawekezaji, jamii na Serikali, kuongeze ajira kwa bodaboda , wajasiriamali wadogowadogo na kukua kwa mji, pia tunaiomba serikali kuimalisha ulinzi na usalama katika mali za wawekezaji katika eneo la stendi.
Imeandalikwa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo
Mtaa wa Bomani
Sanduku la Barua: S.L.P 70
Telephone: 028 2223403
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@biharamulodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya Biharamulo. Haki zote zimehifadhiwa