Mwezeshaji wa TASAF wa Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo Mkoa wa Kagera Leonidas Rwezaura amewataka walengwa wa TASAF kukata bima ya afya kwa kutumia malipo wanayolipwa ili kuweza kupunguza gharama kubwa ambazo wanatumia hospital kwa matibabu.
Rwezaura ameyasema malengo ya TASAF katika Wilaya ya Biharamulo ni kuhakikisha wananusuru kaya masikini kati ya walengwa 5649 katika vijiji 50 ambavyo vimepewa zaidi ya Tsh, milioni 233.
“ Viongozi wa kaya watoe taarifa kamili katika mahudhurio ya shule na kliniki ili kuepusha kupunguzwa kwa malipo wanayopokea”,Amesema Rwezaura.
Nae, mwezeshaji wa TASAF Wilaya ya Biharamulo James Ndyanabo amesisitiza kwenye familia lazima kuwe na ushirikiano na mshikamano ambao utaweza kusaidia matumizi mazuri ya mpango kwa walengwa.
Kwa upande wake Mtendaji wa Kijiji cha Kasuno Kata ya Nyamahanga, Wolfrem Magroce, amesema mara baada ya malipo kufanyika huwa wanaenda kumtembelea kila mmoja nyumbani kwake ili kujiridhisha kama hayo maendeleo wanayoyasema wameyatekeleza
Mwenyekiti wa Kjiji cha Nyabusozi Kata ya Nyabusozii Dominick Antoni, amesema kabla ya zoezi la malipo walienda kujiridhisha kuwa maendeleo ambayo wananchi wao wamefanya kupitia mpango wa TASAF nikweli wamefanya maendeleo makubwa sana katika vijiji tofauti ambavyo vinawalengwa.
Mkazi wa Kijiji cha Nyabusozi Konsolata Rikado mwenye familia ya watoto saba, amesema TASAF imemsaidia sana katika maisha yake ya kawaida ameweza kununua bati nane ambazo amejengea nyumba yake na matumizi ya watoto shuleni anashukuru sana kwa msaada ambao wanaupata kutoka kwenye malipo ya TASAF.
Nae, Fortunatusi Paulo mkazi wa Kijiji cha Kasuno, amesema kupitia TASAF ameweza kununua baiskeli moja, shamba heka moja, kuku watano na bati kumi haya ni matunda ambayo ameyapata kutoka katika malipo ya TASAF.
Imeandaliwa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo
Mtaa wa Bomani
Sanduku la Barua: S.L.P 70
Telephone: 028 2223403
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@biharamulodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya Biharamulo. Haki zote zimehifadhiwa