Mkuu wa idara ya Maendelo ya Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo Mkoa wa Kagera, Mwema Doto Salum amewataka wanavikundi kuwa na usimamizi mzuri wa miradi ambayo wameombea mkopo huo pia kuwa waaminifu katika matumizi mazuri ya fedha iliyotolewa na serikali zaidi Tsh Milioni 97.
Ameyasema hayo 28/4/2021 kabla ya kuanza zoezi la kusainisha mkataba wa mkopo wa robo ya tatu katika vikundi maalum vya kiuchumi na kijamii kwa wanawake, vijana, na watu wenye ulemavu. Mkopo huo unatokana na makusanyo ya asilimia kumi ya ndani ya Halmashauri na kutoa kwa vikundi 25, vikundi vya wanawake ni 17, vijana 6 na vikundi vya wenye ulemavu ni viwili kutoka kata sita ambazo ni Nyarubungo, Biharamulo mjini, Lusahunga, Ruziba, Bisibo na nyakahura.
"Nimuhumu kila kikundi kutunza kumbukumbu katika miradi yao wanayoifanya na kabla ya kuchukua Mkopo ambao wameomba na kikundi kikapata pungufu mna uhuru wa kukataa na kupata ushauri na utaratibu wa kufanya ili waweze kukizi vigezo vya kupata wanacho kitaka".Amesema Salum.
Nae, Afisa vijana wa Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo Godfrey Kajungu amesisitiza kuhusu marejesho ya pesa hizo ni muhim Sana kwa sababu itawasaidia kutoa Mkopo kwa watu wengine wenye uhitaji hata na wao wamepata kutokana na marejesho ya watu wengine ambao wameshapata Mkopo huo na wanavikundi kujiepusha na matumizi ya pesa yasiyo ya lazima na kufanya malengo yaliyowafanya kuomba mkopo huo.
wanavikundi kujiepusha na matimizi ya pesa yasiyo ya lazima na kufanya malengo yaliyowafanya kuomba mkopo huo.
Nae, karibu wa kikundi Cha (UWABI) umojawa wa wanawake Bisibo Geralidina Daudi amesema wanashukuru wao Kama kikundi Cha watu 16 wameweza kufanya Maendelo mbalimbali ya kufuga kuku na kila mwanakiku ameweza kunufaika na mradi huo
Kwa upande wake katibu wa kikundi Cha watu wenye ulemavu kutoka kata ya Bisibo amesema wao wameweza kununua mbuzi nane, walio Jenga katika kikundi chao ni watu watano na walio nunua baisikeli ni watu watatu na matarajio yao kwa mkopo watakao upata awamu hii ni kununua mbuzi 16 na kununua mazao ya nafaka kwa ajiri ya biashara.
Imeandaliwa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo
Mtaa wa Bomani
Sanduku la Barua: S.L.P 70
Telephone: 028 2223403
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@biharamulodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya Biharamulo. Haki zote zimehifadhiwa