Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo Mkoa wa Kagera, Kanali Mathias Kahabi awataka Madiwani kuhamasisha wananchi kuchangia fedha kwa ajili ya maendeo ya jamii na sio kukusanya kwa manufaa yao binafisi pia kufatiria miradi yote inayojengwa katika Kata zao kama inafanyika kwa wakati.
Maagizo hayo ameyatoa katika kikao cha Baraza la Madiwani ambalo limefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo 30/4/2021.
Kahabi amewaagiza Madiwa wahakikishe makusanyo yote ya ndani ya Halmashauri yanakusanywa kwa PoS ili iwasaidie kujua asilimia ya mapato katika Halmashauri imefika kiwango gani pia amewataka madiwani wa Kata tisa ambao makusanyo yao yapo chini sana kuongeza juhudi.
“Lazima tuhoji ninani aliyetufikisha hapa hadi kupata hati chafu katika mapato na Wilaya yetu kuwa ya mwisho Kimkoa”, Amesema Kahabi.
Nae Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo Waziri K. Kombo,ametoa maagizo kwa watendaji ambao wanakusanya mapato bila PoS wakibainika watachukuliwa hatua za kisheria kwa sababu utaratibu uliowekwa na serikali makusanyo yote yanatakiwa kukusanywa kwa njia ya PoS.
“Kuelekea kumaliza mwaka wa fedha hadi sasa Halmashauri imeingiza mapato kwa asilimia 81 ikiwa ni robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2020/21, tumepiga hatua kubwa sana kuliko mwaka uliopita tulikusanya asilimia 63”, Amesema Kombo.
Hata hivyo amewapongeza wasaidizi wake kwa kuongeza juhudi hadi kufikia hatua hii waliopo kwa sasa pia kuwashukuru Madiwani kwa ushirikiano wa kuhamasisha mapato.
Imeandaliwa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo
Mtaa wa Bomani
Sanduku la Barua: S.L.P 70
Telephone: 028 2223403
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@biharamulodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya Biharamulo. Haki zote zimehifadhiwa